Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho
anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400
zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Katibu
Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya
Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017
ikitokea Canada ilikotengenezwa.

EmoticonEmoticon