HAKUNA mbabe, ule mtanange uliokuwa unasuburiwa kwa hamu kubwa
uliohusisha mahasimu wawili Yanga na Simba umemalizika jioni ya leo kwa
timu hizo kutoka sare ya 1-1. Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa kila upande, Yanga
walifanikiwa kupata goli dakika ya 26, baada ya Amisi Tambwe kumzidi
mbinu beki Novat Lufungo wa Simba na kuandika goli la kuongoza huku
nahodha Jonas Mkude akipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi kwa
kudai kuwa Tambwe aliushika mpira kwa mkono. Mpira ulisimama kwa
dakika takribani tano na vurugu kutokea ikiwemo mashabiki wa Simba
kuanza kung'oa viti na kuvirusha uwanjani, hali iliyopelekea Jeshi la
Polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia iliyojitokeza
uwanjani hapo.
Mpaka ilipofika mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa goli 1-0, lakini
kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondan
aliyekuwa na kadi ya njano na kuingia Andrew Vicent "Dante", Saimon
Msuva akachukua nafasi ya Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima akiingia baada
ya Deus Kaseke, Simba wakimtoa Laudit Mavugo na kuingia Fredrick
Blagnon, Ibrahim Ajib na kuingia Mohamed Ibrahim na Novat Lufungo na
kuingia Jurko Murshid. Mchezo uliokuwa wa kasi kwa kila upande huku
Yanga wakitafuta goli la kuongoza na Simba wakisaka la kusawazisha,
ambapo dakika ya 89 Shiza Kichuya anawainua mashabiki wa Simba baada ya
kupiga kona iliyoenda moja kwa moja wavuni na kusawazisha na kudumu
mpaka dakika 90. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya akishangia baada ya kuipatia timu
yake goli la kusawazishi dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga ikiwa ni
mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiipatia timu
Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play
EmoticonEmoticon