Showing posts with label Sport. Show all posts
Showing posts with label Sport. Show all posts

Sunday, October 2, 2016

Simba, Yanga Marufuku Uwanja wa Taifa

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezifungia rasmi timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na Serikali.

Nape ametoa amri hiyo leo Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung'oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.

"Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu," alisema Nape.
Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play

Saturday, October 1, 2016

SIMBA, YANGA ZATOSHANA NGUVU TAIFA LEO, MASHABIKI WANG'OA VITI UWANJANI

 
HAKUNA mbabe, ule mtanange uliokuwa unasuburiwa kwa hamu kubwa uliohusisha mahasimu wawili Yanga na Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa kila upande, Yanga
 
walifanikiwa kupata goli dakika ya 26, baada ya Amisi Tambwe kumzidi mbinu beki Novat Lufungo wa Simba na kuandika goli la kuongoza huku nahodha Jonas Mkude akipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi kwa kudai kuwa Tambwe aliushika mpira kwa mkono.
Mpira ulisimama kwa dakika takribani tano na vurugu kutokea ikiwemo mashabiki wa Simba kuanza kung'oa viti na kuvirusha uwanjani, hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.
 Mpaka ilipofika mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondan aliyekuwa na kadi ya njano na kuingia Andrew Vicent "Dante", Saimon Msuva akachukua nafasi ya Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima akiingia baada ya Deus Kaseke, Simba wakimtoa Laudit Mavugo na kuingia Fredrick Blagnon, Ibrahim Ajib na kuingia Mohamed Ibrahim na Novat Lufungo na kuingia Jurko Murshid.
Mchezo uliokuwa wa kasi kwa kila upande huku Yanga wakitafuta goli la kuongoza na Simba wakisaka la kusawazisha, ambapo dakika ya 89 Shiza Kichuya anawainua mashabiki wa Simba baada ya kupiga kona iliyoenda moja kwa moja wavuni na kusawazisha na kudumu mpaka dakika 90. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 
Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya akishangia baada ya kuipatia timu yake goli la kusawazishi dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiipatia timu
Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play Watch full video Down crick watch video or download Video for free and start watch full video now HD video play